MAMBO YA KUZINGATIA ILI UWE MFANYA BIASHARA MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA

 MAMBO YA KUZINGATIA ILI UWE MFANYA BIASHARA MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA SANA 

Aya ni mambo ya msingi ya  kuzingatia kama wewe ni mfanya biashara ili uweze kua ni mfanya biashara mwenye mafanikio makubwa sana katika maisha yako  akikisha unazingatia mambo aya .

               1.mtangulize MUNGU  wako :

Akikisha  unamtanguliza mungu katika kila jambo ambalo unalolifanya katika maisha yako maana yeye ndio muweza wa kilakitu katika maisha yetu hivyo kama unaitaji Siku moja kua mfanya biashara mwenye mafanikio makubwa sana akikisha unamuomba Mungu sana katika maisha yako maana yeye ndio kakupa pumzi bure na akikisha unamuomba kila siku aweze kukujalia afya bora katika maisha yako ya hapa duniani kwani bila yeye tusinge kuwepo  apa duniani hivyo ndugu yangu akikisha unamuomba kila siku mungu wako ambaye unamuamini katika maisha yako kama ni muislam,msabato,mroma  n.k

Akikisha unamuomba kila siku mungu wako akubaliki,akufanye usikate tamaa , n.k

                  2.penda sana kujifunza  kila siku maarifa mapya :

Wafanya biashara wote wenye mafanikio makubwa sana ni watu ambao  sana penda kujifunza maarifa mapya kila siku katika biashara wanazo zifanya na vitu wanavyo vifanya kwani kwa kujifunza maarifa mapya kila siku inasababisha ubongo uwe " creativity " yaani ufumbuzi na pia kupitia kujifunza  maarifa mapya kila siku inasababisha mtu aweze na ujuzi mkubwa kupitia kile kitu ambacho yeye anakifanya .hivyo  kama unapenda kua mfanya biashara mwenye mafanikio katika maisha yako akikisha una penda kujifunza mambo mapya kila siku katika maisha yako jifunze kupitia kusoma vitabu mbalimbali  kuusiana na mifanio.

              3.Usiache kutangaza biashara yako :

Biashara yoyote ile ili iweze kukua nilazima iwe inatangazwa pasipo kuitangaza biashara  haitaweza kukua hivyo kama wewe ni mfanya biashara akikisha hauachi kutangaza biashara yako kwani kwa kufanya hivyo utaweza kupata wateja wengi katika biashara yako na kitu ambacho kitapelekea uwe mfanya biashara mwenye mafanikio makubwa   na kwakuitangaza biashara yako ita sababisha uatu wahifahamu  zaidi biashara yako katika maeneo mbalimbali kote duniani na Tanzania pia utazidi Ku I brand biashara yako na hapo watu wengi wanafanya makosa pindi biashara zao zinapo anza kupata mafanikio Fulani basi wanaacha kutangaza biashara zao na hapo ndipo wanapo Fanya makosa kwani wana shindwa kupata wateja wengine wapya ushawai kujiuliza kwanini makampuni kama vile vodacom ,tigo,NMB,CRDB, n.k licha ya mafanikio waliyo nayo bado hawaachi kutangaza biashara zao wana Fanya hivyo ili kuvutia wateja wapya

                 4.Kua mkweli kwa wateja wako:

Kila mtu apa duniani anapenda kuambiwa ukweli hivyo ata wateja wana itaji ukweli hivyo kama unaitaji Kua mfanya biashara mwenye mafanikio makubwa akikisha unakua mkweli kwa wateja wako kwani ukweli pekee umuweka mtu huru kama bizaa ni bora waambie ukweli , usipende sana kuwadanganya wateja wako kwani kwa kufanya hivyo utasababisha wateja wengi wakukimbie hivyo akikisha unakua mkweli kwa wateja wako ili uweze Kua mfanya biashara mwenye mafanikio makubwa sana

                 5.Akikisha unaunda  team ya watu ambao utafanya nao kazi wawe watu ambao unawaamini :

Ili uweze kupata mafanikio makubwa katika kitu chochote kile ambacho unakifanya ni lazima uwe na team ya watu ambao watakua wana kusaidia shuguli mbalimbali za biashara yako au kampuni yako mfano wafanya biashara wote wenye mafanikio wanao watu ambao wanashilikiana katika shuguli mbalimbali  mfano mzuri ni mo na wafanya biashara wengine wengi wanao watu ambao wana shilikiana nao katika shuguli mbalimbali kama vile kufanya maamuzi mbalimbali na mambo mengineyo mengi mesali isemavyo 

"Umoja ni nguvu na utengano ni uzaifu " hivyo ili uweze kufanikiwa katika kwa viwango vikubwa  akikisha unaunda team ambayo itakua inakusaidia katika majukumu mbalimbali katika kampuni au katika biashara hiyo





            6.Usiogope  kufeli katika biashara :

Kitu chochote katika dunia hii ili kiweze kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kunawakati lazima kinafeli  ata mtoto anapo jifunza kutembea kunawakati ana anguka lakini hakati tamaa hivyo hivyo katika biashara ili uweze kufanikiwa  lazima kuna wakati utafeli katika biashara yako hivyo hautakiwi kuogopa kufeli katika biashara kwani ukiona hauja wai kufeli katika biashara yako au katika maisha yako jua kwamba haujawai jaribu kitu chochote  katika maisha yako .usiogope kufeli kwani kufeli ndio njia ya mafanikio katika maisha yako katika  biashara yako katika kampuni yako  .ili uweze kufanikiwa kwa viwando vikubwa katika biashara yako au katika kampuni yako au katika maisha yako ni lazima kufeli Mara nyingi

Na unapo feli usikate tamaa endelea kupambana na endelea kusonga mbele



                7.penda sana kujitofautisha na watu wengine katika mfumo  wa utoaji uduma ;

Ili uweze kufanikiwa katika biashara yako kwa viwango vikubwa sana akikisha unapenda sana kujitofautisha na wafanya biashara wengine katika mfumo wa utoaji huduma kwani kwa kufanya hivyo utaweza kuwa vutia wateja wengi katika biashara yako  unatakiwa kutafuta kitu ambacho ukikifanya kitakutofautisha na watu wengine na kita fanya wateja wengi waje katika biashara yako au katika kampuni yako .mfano mteja akinunua mzigo mkubwa anapele kewa mbaka anapo kaa  n.k




Comments

Popular posts from this blog

SHERIA ZA BIASHARA