SIRI YA MAFANIKIO
Baada ya kusoma kitabu cha LAW OF MAKING MONEY kilicho andikwa na BRIAN TRACY hiki kitabu kinaelezea sheria za kutengeneza fedha au kupata fedha na katika sheria izo ni
PARKINSON'S LAW : watu wengi sana wanaitumia sheria hii pasipo wenyewe kujua na wengine wanaijua ila awajui kama ni kikwazo kikubwa sana cha mafanikio katika suala zima la fedha katika maisha yao
Hii sheria inasema kwamba pindi ambapo kipato cha mtu kinaongezeka na matumizi ya mtu uyo yanaongezeka Mfano mwalimu ambaye alikua analipwa shilingi laki tatu na akaona fedha izo ni ndogo na anashindwa kutimiza malengo yake kwa sababu fedha aliyo kua anaipata inaishia kwenye matumizi hivyo akaamua kwenda kuongeza elimu ili aweze kupandishiwa mshahara na aweze kutimiza malengo yake na pindi alipo ongeza elimu na mshahara wake ukaongezeka lakini akashangaa bado fedha anayo ipata ina isha yote na anashindwa kutimiza malengo yake. Kwa sababu ya sheria hii ya "Parkinson's law pindi ambapo samani ya mtu inaongezeka na matumizi ya mtu uyo yana ongezeka au pindi ambapo kipata cha mtu kinaongezeka na matumizi ya mtu uyo yana ongezeka
Kwaiyo kipato cha mtu = na matumizi ya mtu uyo
Hivyo hivyo
Pindi ambapo samani ya mtu inaongezeka na matumizi yake yanaongezeka
Hivyo ili uweze kufanikiwa katika maisha yako akikisha unaivunja sheria hii ya PARKINSON'S LAW kwa kupunguza matumizi yako mfano unaingiza elfu kumi kwa siku akikisha matumizi yako ni chini ya elfu kumi namaanisha elfu tano na nyingine kawekeze ila pasipo kufanya ivyo kufanikiwa katika suala zima la fedha itakua ni ngumu sana ivyo akikisha unavunja hii sheria ndipo uweze kufanikiwa
Pia atakama samani yako ikiongezeka akikisha unapunguza matumizi yako na sio kuongeza matumizi mfano unataka umiliki gari la kifahari kisa umeongezewa mshahara au unataka kuishi maisha ya kifahari kisa kipato chako kimeongezeka unatakiwa kupunguza matumizi yako na fedha nyingine nenda kawekeze kwa kufanya hivyo utaweza kufanikiwa katika suala zima la fedha
Comments
Post a Comment