SIRI ZA MAFANIKO

 SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA EPISODE :01

              Kuna siri mbalimbali ambazo zime wafanya watu wenye mafanikio mfano ,jack ma ,jeff bezos,bill gates, na wengineo wengi waweze kufanikiwa katika maisha yao na Leo naenda Ku share na wewe siri za mafanikio katika maisha na kama ukizifuata siri hizi na hakika utaenda kubadilisha maisha yako na utaweza kufanikiwa

                     1.Kua na malengo au ndoto : watu wote wenye mafanikio duniani wana malengo   ambayo yanawaongoza wenyewe nini cha kufanya katika dunia hii kwa sababu kuna mambo mengi duniani ya kufanya kwaiyo usipo kua na malengo ya nini ambacho unakiitaji itakua ni ngumu sana kwa wewe kufanikiwa kwa sababu utakua ujui mahali unapo enda  mfano mtu ambaye ajui mahali anapo enda kwaiyo mahali popote atakapo fika atajua amefika








 Faida za kua na malengo

      ____ malengo yana kusaidia  kuweka vipao mbele katika maisha yako

    _____malengo yana kusaidia wewe kujichagulia maisha ambayo wewe unaitaji kuyaishi kwa maana ukishindwa kujichagulia maisha  ambayo unaitaji kuyaishi  basi maisha yenyewe  yatakuchagulia  maisha sahihi ya wewe kuishi mfano watu wengi ni waizi ,walevi, wabakaji,wavuta bangi,matapeli ,wa vivu  n.k

Hiyo yote ni sababu walishindwa kujichagulia maisha sahihi ya wenyewe kuishi na awakua na malengo katika maisha yao hivyo maisha yenyewe yakawachagulia maisha sahihi ya wenyewe kuishi na maisha ayo uwa ni mabaya  maisha yasio na furaha ,maisha ya kuzaraulika ,maisha ya umaskini 

  Ivyo kama unaitaji mafanikio katika maisha yako basi akikisha unakua na malengo  ya nini ambacho unakiitaji katika dunia hii au nini ambacho unakiitaji kukifanya katika dunia hii  usiishi bora kuishi  ishi kwa malengo jiwekee malengo yako na kama hauna  malengo basi akikisha Leo hii baada ya kusoma nakala hii unatafakali nini ambacho unakiitaji kukifanya katika dunia hii au nini ambacho unakiitaji .








Malengo katika maisha ya mwana damu ni kitu muhimu sana kwa maana malengo au ndoto ndio ambazo umuongoza mtu ni nini cha kufanya na wakati gani afanye na malengo mda mwingine na chukuliaga kama dereva na wewe ni kama gari hivyo wewe ukiwashwa pasipo dereva utapotea na kupata ajari  lakini ukiwa na dereva sio lahisi kupata ajari na kupotea hivyo jitaidi sana kua na malengo katika maisha yako


               2.Amini katika malengo yako au ndoto yako :  hii ni siri namba mbili unatakiwa kuamini ndoto yako  ukishindwa kuamini ndoto yako au malengo yako itakua ni ngumu sana kwa wewe kufanikiwa  kwa sababu unafanya kitu ambacho wewe mwenyewe hauna uwakika nacho kwaiyo itakua ni ngumu sana kwa icho kitu kutokea katika maisha yako ivyo watu wote wenye mafanikio duniani ni watu ambao wanaamini sana katika ndoto zao au malengo yako

Hivyo kama wewe unaitaji mafanikio katika maisha yako akikisha unaamini  sana ndoto zako au malengo yako kwa kufanya hivyo utaweza kufanikiwa katika maisha yako siku moja wewe endelea kuamini katika ndoto zao au malengo yako atakama ni makubwa kiasi gani wewe endelea kuamini tu mfano una ndoto ya kufungua kampuni lakini saizi auna ata mia wewe endelea kuamini tu katika ndoto yako au malengo yako ipo siku yata kua kweli tu.









Ili uweze kufanikiwa katika maisha ni lazima uwe na imani kubwa ya kuiamini ndoto yako au malengo yako kama siku moja yata timia  na kweli yatatimia ila ukiamini kwamba ayata timia na kweli ayata timia

Ivyo watu wote wenye mafanikio wanaamini sana katika ndoto zao kwamba zita kamilika

Hivyo kua na imani katika ndoto yako na amini siku moja zitakua kweli


                 3.Uvumilivu : Mafanikio ni process ndefu (mchakato mrefu)  sio kitendo cha kulala maskini na kuamka tajili Bali mafanikio yana chukua mda sana na hii ndio sababu kubwa sana watu wengi wanashindwa kutimiza malengo yao sababu wanaitaji mafanikio ya haraka  ya Ku lala maskini na kuamka tajili na ndomana katika asilimia 100% ya watu wote duniani ni asilimia  1% tu ndio ambao wamefanikiwa  lakini walio baki 99% ni watu wenye maisha ya kawaida na maskini kabisa sababu kubwa watu wengi hawana uvumilivu katika vitu ambavyo wana vifanya wanaitaji mafanikio ya haraka sana na ndio maana vifo saizi vimeongezeka sababu watu wengi wana penda njia za mkato watu wana uwana kisa wapate mafanikio ya haraka  na Leo binadamu anamuogopa binadamu mwenzie na ngoja nikwambie ndugu yangu ukifanikiwa kwa njia za mkato mafanikio ayo ayata  dumu na wewe pia auta dumu  

Hivyo kama unaitaji mafanikio katika maisha yako akikisha unakua mvumilivu katika maisha yako







      

Uvumilivu katika kila jambo katika maisha ni muhimu ivyoivyo katika maisha ya mafanikio unatakiwa uwe mvumilivu kwa maana mafanikio ayaji kwa siku moja bali uchukua mda sana hivyo watu wenye mafanikio ni watu ambao wanauvumilivu mkubwa katika maisha yao



       4. Muombe sana Mungu wako : watu wenye mafanikio ni watu ambao wana muomba sana mungu katika maisha ayo kwa maana mwenyezi mungu ndio kilakitu katika maisha yetu hivyo yatupasa kumuomba sana yeye maana ndiye anaye tupa pumzi ,na yeye ndie aliye kufanya wewe mbaka leo ni mzima kabisa na mwenyewe afya tele na ndiye aliye ni Fanya Mimi leo hii ni mzima kabisa hivyo muombea sana yeye maana yeye ndiye muweza wa kila kitu katika maisha yetu.

Muombe sana mungu wako na muamini sana yeye maana yeye ndie muweza wa kilakitu katika maisha yetu watu wenye mafanikio wana muamini sana mungu na wana amini yeye ni muweza wa kila kitu katika maisha yao


        5. Chukua atua katika  malengo yako :

Kua na malengo tu katika maisha au kua na ndoto tu katika maisha haitoshi unatakiwa uchukue atua katika malengo yako au katika ndoto zako kwani kwa kufanya hivyo utaweza kufanikiwa katika maisha yako lakini ukiwa ni mtu ambaye hauchukui hatua katika malengo yako au katika ndoto zako itakua ni ngumu sana kwa wewe kufanikiwa katika maisha yako kunawale wengine wanasema  nitaanza mbaka mambo yakae sawa au nitaanza biashara mbaka nipate mtaji wa million moja  ndugu yangu unatakiwa kuanza hivyo hivyo na ichoicho kidogo ulicho kua nacho kwa maana ata m buyu ulianza kama mchicha lakini leo hii ni mkubwa sana unatakiwa uanze chini ndipo uende juu anza na kidogo ili uweze kupata kikubwa  hivyo chukua hatua sasa  kuanza kupambania malengo yako au ndoto zako na utaweza kufanikiwa katika maisha yako pia anza na ichoicho ulicho nacho


Watu wote duniani wenye mafanikio makubwa ni watu ambao wana chukua hatua mapema katika malengo yao au ndoto zao na  icho ndo kinawafanya wenyewe waweze kufanikiwa katika maisha yao

            6.Penda unacho  kifanya : watu wote wenye mafanikio duniani ni watu ambao wana penda vitu ambavyo wana vifanya yaweza kua katika biashara ,katika kampuni  n.k ni watu ambao wana vipenda vile ambavyo wana vifanya  mfano mo ,bill gates ,Jeff bezos , jack ma ,n.k ni watu ambao licha ya utajili wao uwo wote ni watu ambao bado wanaendelea kwenda ofisini na kufanya kazi ni kwa sababu wana penda vitu wanavyo vifanya hivyo ili uweze kufanikiwa katika maisha yako akikisha unapenda kitu ambacho unakifanya katika maisha yako 

   FAIDA ZA KUPENDA KITU AMBACHO UNAKIFANYA 

       _____Itakua ni ngumu sana kwa wewe kukata tamaa pindi ambapo mambo yana kuwa ayapo sawa kwa sababu katika kuelekea katika mafanikio kunawakati utapitia mgumu ya kupasa wewe usikate tamaa lakini  ukiwa unafanya kitu ambacho ata wewe mwenyewe hukipendi itakua ni rahisi sana kwa wewe kukata tamaa pindi mambo yanapo kua ayapo sawa.

     ______Itakua ni ngumu sana kwa wewe kuchoka katika kitu ambacho unakifanya kwa sababu unakipenda hivyo utafanya zaidi na utafanya isivyo vya kawaida kwa sababu una mapenzi ya zati naicho kitu ambacho unakifanya. Na pia Fanya kitu ambacho wewe unakipenda ndipo utaweza kufanikiwa katika maisha yako.


Pasipo kufanya  hivyo itakua ni ngumu sana kwa wewe kufanikiwa katika maisha yako kwa sababu unafanya kitu  ambacho ata  wewe  mwenyewe aukipendi hivyo utakua unafanya bora riende tu na utakua haufanyi kwa ubora mkubwa sana  hivyo akikisha unakipenda kile kitu ambacho unakifanya  hapo ndipo uta weza kufanikiwa katika maisha yako.

                 Kwa Leo ninge penda kuishia hapo na katika Episode inayo fuata nitaenda kumalizia siri za watu wenye mafanikio 

PIA KWA TAARIFA ZAIDI NA KWA MAFUNZO ZAIDI TAZAMA VIDEO IZO APO CHINI ILI UWEZE KUJIFUNZA ZAIDI  PIA USISAHAU KU SUBSCRIBE KATIKA CHANNEL YETU NA MUNGU AKUBALIKI NDUGU YANGU 








TAFAZALI SUBSCRIBE KATIKA CHANNEL YETU YA YOUTUBE KWA  TAALIFA ZAIDI NA VIDEO ZAIDI   ASANTE

Mimi kwa majina naitwa : Denis Jenson
YouTube : Denis Jenson
No. 0765911413



Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YA KUZINGATIA ILI UWE MFANYA BIASHARA MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA

SHERIA ZA BIASHARA