TABIA ZINAZO KUFANYA UWE MASKINI KATIKA MAISHA YAKO. Episode :1

 TABIA ZINAZO KUFANYA UWE MASKINI KATIKA MAISHA YAKO.

                Katika suala Zuma lakufanikiwa au kutofanikiwa katika maisha inategemeana na tabia ambazo mtu ana kua akiziishi katika maisha yake .hivyo ukiona mtu amefanikiwa katika maisha yake basi ujue kuna tabia  ambazo mtu uyo mwenye mafanikio alikua akiziishi na zika mpelekea yeye kufanikiwa na ukiona mtu ambaye ajafanikiwa katika maisha yake basi ujue kuna tabia ambazo alikua akiziishi na zika mfanya yeye awe maskini  hivyo

Na baada ya uchunguzi wa mda mrefu nimekuja ku baini tabia ambazo zina mfanya mtu awe maskini katika maisha yake na kama akiweza kuacha tabia izi basi ata weza kufanikiwa katika maisha yake na kuishi  maisha ya ndoto zake Kuna tabia nyingi ambazo zinaweza kumfanya mtu akawa maskini katika maisha yake  na leo ninge penda Ku share na wewe tabia (30) ambazo zina kufanya uwe maskini katika maisha yako na ukiweza kubadili tabia izi na Kuakikishai utaweza kua mtu mwenye mafanikio katika maisha yako yote 


                 1.TABIA YA ULEVI :

Ukiwa na tabia hii ya ulevi itakua ni ngumu sana kwa wewe kufanikiwa katika maisha yako kwa sababu fedha zote ambazo utakua unazipata zitakua zinaishia kwenye pombe ngoja nikupe mfano mdogo tu mtu kila siku ana kunywa pombe chupa tano  na kila chupa ya bia ni elfu  2000/=   tupige hesabu ndogo tu 

 Mwaka unasiku 360 zidisha kwa chupa tano ambazo mtu ana kunywa kila siku

360 ×5=1800 

Hivyo ata kua amekunywa chupa 1800

Zidisha kwa elfu mbili 2000/= ambayo ni bei ya bia moja au pombe yoyote ile ambayo unakunywa ili uweze kupata kwa mwaka unatumia kiasi gani

1800×2000=3600000/=

Hivyo kwa mwaka ana tumia milioni tatu na laki sita (3600000/=)  

Hivyo unajikuta unatumia fedha nyingi katika ulevi na wakati fedha iyo ungeenda kuwekeza unge kua mbali sana kiuchumi au iyo milioni tatu ungewekeza katika biashara , katika kilimo au unge nunua pikipiki na kuwapa watu wafanyie kazia na wewe wana kulipa fedha kila wiki au kila siku au unge nunua guta ambayo unge kua unatumia kubebea mizigo

Pia ulevi zio mzuri kiafya kwani umu zoofisha mtu na kumfanya aonekane mzee kumbe kijana kabisa .hivyo kama unatabia hii ya ulevi acha au anza kwa kupunguza kiasi ambacho unakunya kila siku .kwa sababu mtu ukiwa mlevi ata jamii ambayo utakua unaishi auta weza kueshimika hivyo achana na ulevi kabisa ili uweze kufanikiwa kwani ni kikwazo cha mafanikio yako katika maisha yako.


     Hivyo kama wewe unatabia hii tafadhari acha Mara moja kwani ni kikwazo kikubwa cha mafanikio katika maisha yako.


       2.TABIA YA KUKATA TAMAA :

Watu wengi wana shindwa kufanikiwa katika maisha yao sababu ni watu ambao wana kata tamaa katika maisha yao ukiwa ni mtu ambaye una kata tamaa mapema katika maisha yako itakua ni suala gumu sana kwa wewe kufanikiwa katika maisha yake kwa sababu kitu ukianza kufanya kitu kwa Mara ya kwanza kitu hicho akiwezi kufanikiwa hivyo au takiwi kukata tamaa katika maisha yako 

WARREN BUFFETT  : 

Ana sema 

"Aijalishi upo vizuri kiasi gani kufanya jambo Fulani kuna baazi ya mambo ni lazima ya chukue mda  "

Pia "wezi kupata mtoto kwa siku moja ata kama  ukiwapa mimba wanawake tisa kwa siku moja"

Hivyo autakiwi kukata tamaa katika maisha yako aijalishi unapitia wakati mgumu kiasi gani autakiwi kukata tamaa kwani ukikubali kukata tamaa katika maisha yako umekubali kua maskini watu wote ambao unawaona wenye mafanikio ni watu ambao hawakukata tamaa katika maisha yao.

Hivyo kama wewe unaitaji mafanikio katika maisha yako hautakiwi kukata tamaa katika maisha yako.


Hivyo kama wewe unatabia hii tafadhari acha Mara moja kwani ni kikwazo kikubwa cha mafanikio  katika maisha yako.

            3.TABIA YA KUTO JIWEKEA AKIBA KATIKA MAISHA YAKO :

Akiba ni kitu cha msingi sana katika maisha ya mwanadamu kwani itaweza kumsaidia pindi ambapo ata patwa na tatizo fulani au pindi ambapo itatokea fursa Fulani katika maisha yake ambayo itakua inaitaji fedha itakua ni rahisi sana kwa mtu ambaye ana jiwekea akiba kuweza kuwekeza katika eneo hilo  na kuweza kujipatia faida kubwa sana katika maisha yake hivyo kama hauna utamaduni wakujiwekea akiba katika maisha yako basi anza sasa kama ni mfanya kazi akikisha kila ambapo utapata mshahara basi  unajiwekea akiba kwani kwa kufanya ivyo ita kua ni lahisi sana kwa wewe kufanikiwa katika maisha yako anza ata kwa kujiwekea akiba asilimia 10% kila ambapo uta pata mshahara na amini ukianza kwa kujiwekea akiba asili mia 10% utakapo anza kupata faida tu utaanza kuongeza kiwango cha kujiwekea akiba  .hivyo akiba ni kitu cha muhimu katika maisha kama unaitaji mafanikio.



           Hivyo kama wewe unatabia hii tafadhari acha Mara moja kwani ni kikwazo kikubwa cha mafanikio  katika maisha yako.


TAZAMA VIDEO HII ILI UWEZE KUJIFUNZA  ZAIDI PIA USISAHAU KU

1.SUBSCRIBE NA KU BOFYA ALAMA YA KENGELE KATIKA CHANNEL YETU ILI USIPITWE NA VIDEO ZAIDI KUHUSU MAFANIKIO

2.LIKE ,COMMENT NA PIA USISAHAU KU SHARE VIDEO HII ILI NA WENGINE WAWEZE KUJIFUNZA ZAIDI.

ASANTE




Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YA KUZINGATIA ILI UWE MFANYA BIASHARA MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA

SHERIA ZA BIASHARA